Majlisi ilijaa hisia za Mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s) na huzuni kubwa ya kuuawa Kishahidi kwa Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake katika Ardhi ya Karbala, kupitia muovu na mlaaniwa Yazid bin Muawia (la) na majeshi yake.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii Maombolezo ya Shahada ya Imam Hussein (a.s) yameendelea Nchini Iran katika Husayniyya ya Imam Khomeini (r.a).
Maombolezo haya ya kiroho na yenye baraka kwa ajili ya kumkumbuka Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein (a.s), kama ilivyo desturi ya kila mwaka, yanafanyika katika Husayniyya hii ya Imam Khomeini (r.a) katika siku za Mwezi Mzima wa Muharram.
Katika Picha, Majlisi hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Familia za Mashahidi, na Waumini kutoka matabaka mbalimbali ya jamii.
Marasimu hii ilihusisha usomaji wa Qur’an Tukufu, Khutba katika Mnasaba husika, na Maombolezo kwa Mashairi ya Huzuni kuhusiana na tukio la Karbala.
Majlisi ilijaa hisia za Mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s) na huzuni kubwa ya kuuawa Kishahidi kwa Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake katika Ardhi ya Karbala, kupitia muovu na mlaaniwa Yazid bin Muawia (la) na majeshi yake.
Katika nyuso za Waumini, Mapenzi ya dhati kwa Ahlul-Bayt (a.s) yalionekana wazi, na ujumbe wa A'shura - yaani kusimama dhidi ya dhulma na kulinda Dini Tukufu - uliwasilishwa kwa namna ya wazi na yenye nguvu na hamasa kubwa.
Your Comment